Wednesday, June 3, 2026

Top Stories

View all
SERIKALI YAANZA KUJENGA KITUO CHA ASKARI WA WANYAMAPORI WILAYANI TUNDURU ILI KUDHIBITI TEMBO

SERIKALI YAANZA KUJENGA KITUO CHA ASKARI WA WANYAMAPORI WILAYANI TUNDURU ILI KUDHIBITI TEMBO

Afisa Wanyamapori wilaya ya Tunduru Limbega Hassan akitoa taarifa ya matukio ya wanyamapori waharibifu kwa Mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro(hayupo pichani)aliyetembelea ujenzi wa kituo cha askari wa wanyamapori kinachojengwa katika kijiji cha Chingulungulu kata ya Muhuwesi. Kaimu Mkuu wa idara ya maliasili na mazingira  wilaya ya Tunduru Omben Hingi akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo cha askari wa wanyamapori kwa Mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro wa pili kushoto kinachojengwa katika Chingulungulu wilayani humo. Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro akizungumza na viongozi wa kijiji cha Chingulungulu na kata ya Muhuwesi alipotembelea kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kituo cha askari wa wanyamapori katika kijiji cha Chingulungulu wilayani humo. Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Julius Mtatiro, akisikiliza maelezo ya ujenzi wa kituo cha askari wa wanyamapori kutoka kwa fundi wa mradi huo Shaban Allai wakati mkuu huyo wa wilaya alipotembelea kuangalia ujenzi wake. Picha zote na Muhidin Amri ……………….. Na Muhidin Amri, Tunduru SERIKALI kupitia mamlaka ya usimamizi wanyapori Tanzania(Tawa) kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya Tunduru,imeanza kujenga kituo kikubwa  cha  askari wa wanyamapori ili kudhibiti wanyama wakali na waharibifu wanaovamia makazi ya watu na kuharibu mazao mashambani. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa idara ya maliasili na hifadhi ya mazingira wilaya ya Tunduru Ombeni Hingi,kwa mkuu wa wilaya  hiyo Julius Mtatiro aliyetembelea ujenzi wa kituo hicho kinachojengwa  katika kijiji cha Chingulungulu kata ya Muhuwesi. Hingi alisema,lengo la kujenga kituo  hicho ni katika jitihada za Serikali  za kudhibiti na kukabiliana na changamoto kubwa  ya wanyama  hao hasa Tembo  wanaotoka porini na kwenda kwenye makazi ya watu. Alisema,wilaya ya Tunduru ni miongoni mwa maeneo yenye changamoto kubwa ya wanyama wanaohatarisha maisha ya watu na kuharibu mashamba,hivyo Serikali imeona ni vyema kujenga kituo hicho ambacho kitakuwa na askari watakaofanya kazi ya kudhibiti wanyama hao. Kwa mujibu wa Hingi,walifanya jitihada mbalimbali kuomba msaada katika taasisi,idara za Serikali na  zisizo za Serikali ili kuwasaidia kukabiliana na wanyama hao,lakini wizara ya maliasili na utalii kupitia Tawa ndiyo waliokubali kutoa  Sh.milioni 80 kwa ajili ya kujenga kituo hicho. Alisema,kwa sasa  Halmashauri ya wilaya  Tunduru kupitia idara ya  maliasili inakabiliwa na changamoto kubwa ya vitendea  kazi na watumishi ambao wako tisa(9) tu hivyo ,hawawezi kutokana na tatizo kubwa la wanyama  hao katika wilaya ya Tunduru. Alisema,kujengwa kwa kituo hicho na vituo vingine vidogo vitakavyojengwa hapo baadaye ambavyo vitakuwa na askari wengi kutaongeza nguvu katika jitihada za kukabiliana na wanyamapori. Kwa upande wake Afisa Wanyamapori wa wilaya  hiyo Limbega Hassan alisema,kijiji cha Chingulungulu na kata ya Muhesi ni maeneo yenye changamoto kubwa ya kuvamiwa na wanyamapori mara kwa mara. Alisema,kujengwa kwa kituo hicho katika kijiji hicho ni kama bahati kwani kuna maeneo mengi yenye uhitaji wa askari wa wanyamapori  na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa askari watakaoletwa ili waweze kutekeleza majukumu yao  badala ya kuwaogopa. Diwani wa kata ya Muhuwesi Imani Ngonyani amehaidi kutoa ushirikiano wa hali na mali  kwa fundi aliyepewa kazi ya kujenga kituo hicho na hata kwa askari watakaoletwa kwa ajili ya kusaidia wananchi kukabiliana na wanyama hao. Mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro,ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa usikivu wake na kuleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Tunduru  katika kudhibiti matukio ya kushambuliwa na Tembo. Alisema,tatizo la wananchi kushambuliwa na tembo katika maeneo yao limekuwa kubwa kutokana na wilaya hiyo kwa sehemu kubwa kuzungukwa na Hifadhi ya Nyerere yenye wanyama wengi wakali na waharibifu wa mazao.…

WAKUU WA SHULE WAPEWA MAAGIZO MAZITO

WAKUU WA SHULE WAPEWA MAAGIZO MAZITO

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Profesa Riziki Shemdoe (mwenye suti nyeusi na tai katikati) akiwa katika picha…

ZORAN MAKI KOCHA MPYA SIMBA SC

ZORAN MAKI KOCHA MPYA SIMBA SC

*********** Klabu ya Simba imemtangaza Zoran Manojlovic (Zoran Maki) raia wa Serbia ?? kuwa kocha mkuu wa timu hiyo akichukua mikoba ya Pablo Franco.…