Dar es Salaam, Julai 2, 2026
Watanzania wanne wamejishindia tiketi za safari ya kwenda Mexico kushuhudia mechi za Kombe la Dunia kupitia kampeni ya “Kila Muamala ni Bao la Ushindi”, huku kampuni ya Mixx ikisema kampeni hiyo imeendelea kuongeza matumizi ya huduma za fedha kidijitali nchini.
Washindi hao, waliotoka katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Zanzibar na Arusha, walikabidhiwa tiketi zao katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Bi. Angelica Pesha, alisema kampeni hiyo imeonyesha kuwa huduma za fedha kidijitali zinaweza kuwa zaidi ya njia ya kufanya miamala, kwa kuwa pia zinafungua fursa kwa wananchi.
“Kila muamala una thamani. Unarahisisha maisha ya kila siku, unaongeza usalama wa fedha, unasaidia biashara kukua na leo umefungua fursa kwa baadhi ya Watanzania kwenda kushuhudia Kombe la Dunia nchini Mexico.
Huu ndio ujumbe wa kampeni yetu ya Kila Muamala ni Bao la Ushindi,” alisema Pesha.Alisema hadi sasa zaidi ya washindi 60 tayari wamenufaika kupitia kampeni hiyo kwa kujishindia fedha taslimu, vifaa vya kielektroniki kutoka Hisense pamoja na safari ya kwenda kushuhudia Kombe la Dunia.Mmoja wa washindi, John Mzee, alisema hakutarajia matumizi yake ya kawaida ya Mixx yangemwezesha kutimiza ndoto ya kushuhudia Kombe la Dunia.
“Ninawashukuru Mixx kwa fursa hii ya kipekee. Sikuwahi kufikiria kuwa kufanya miamala yangu ya kila siku kungeweza kunipeleka Mexico. Hii imenithibitishia kuwa kweli kila muamala unaweza kubadilisha maisha,” alisema Mkambala.Pesha alisema kampeni hiyo bado inaendelea, huku washindi wa Shilingi milioni moja wakiendelea kupatikana kila wiki na mshindi mmoja mkuu akitarajiwa kujishindia Shilingi milioni 50.
Aliwahimiza Watanzania kuendelea kutumia Mixx kutuma na kupokea fedha, kulipa bili na kufanya malipo mbalimbali, akisema kila muamala unachangia kuimarisha matumizi ya huduma za fedha kidijitali na kuongeza ujumuishaji wa kifedha nchini.

