WAZIRI wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda, ameitaka Tume ya Taifa ya sayansi na Teknolojia (COSTECH), kutafakari na kufanya tahmini ya kiutendaji, ikiadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwake.

Profesa Mkenda aliyasema hayo Dar es Salaam jana akizindua maazinisho hayo yaliyoanza jana ambayo yatafikia ukomo Oktoba mwaka huu.

Alisema, maadhimisho hayo watayatumia kwa kujisaili wao wenyewe kwamba katika kipindi cha miaka 40, Costech imechangia kiasi gani katika maendeleo ya nchi yetu.

Alisema suala la Sayansi na Teknolojia ni la kutafuta majawabu ,suluhisho na kuhakikisha kwamba wanakwenda kuondoa changamoto katika maisha ya watu.

“Tutatumia kipindi hiki kutafakari vizuri ,tumetumiaje Costech, Costech imetumikaje na imefanya nini kuhakikisha inatatua changamoto za watu” alisema Profesa Mkenda

“Tutaangalia suala la Sayansi na Teknolojia , na teknolojia kama ilivyo,mfano eneo la kilimo ambapo changamoto kubwa ni tija ndogo yaani unapata kiasi gani katika eneo unalolima na kwanini baadhi ya mazao tukilima sisi yanakuwa gharama kubwa kuliko tukiagiza nje” alisema Profesa Mkenda.

Alisema hilo ni suala la Sayansi na Teknolojia kwamba sisi tulimeje kwa udongo wetu ,kwa mbolea ipo ili tuvune vizuri.

Alisema sayansi si ramli bali ni utaratibu ambao ukifanyika mahali popote matokeo yanabaki yaleyale.

Kwaupande wake Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk. Amos Nungu alisema katika maadhimisho hayo yanaenda sambamba na uzinduzi wa mfumo wa kuchukua takwimu za utafiti na Teknolojia.

Alisema Costech ilianzishwa mwaka 1986, ambapo wamekuwa wakitekeleza majukumu mbalimbali ya serikali ya kuratibu masuala yote ya sayansi Teknolojia na ubunifu.

Alisema maadhimisho hayo yatafanyika kwa miezi mitatu kuanzia Julai hadi Oktoba mwaka huu, ambapo kutakuwa na matukio mbalimbali wakihusisha jamii kufanya tathmini walikotoka, walipo na wanakokwenda wakiangalia dira ya taifa 2050.

“Oktoba kutakuwa na mkutano mkuu tutafanya majumuisho ,tutazindua na kitabu tukianza marais wetukutoa sifa zao katika masuala ya sayansi na ubunifu piaatathimi wa vitu mbalimbali ambao wamechangia Costech katika miaka hii ya 40” alisema.