Morogoro, Tarehe 06 Agosti 2026.
Katibu tawala wa Mkoa wa Tanga, Bw. Rashid Mchatta avutiwa na sayansi ya hali ya hewa, aliyasema hayo Tarehe 06 Agosti 2026 mara baada ya kupokea elimu ya hali ya hewa iliyokuwa inatolewa na wataalamu Bingwa wa Hali ya Hewa katika Jengo la Mamlaka lililopo katika Viwanja vya NaneNane, Morogoro kupitia maonesho ya NaneNane yanayoendelea kufanyika kuanzia tarehe 01 hadi 08 Agosti 2026.
“Sayansi ya hali ya hewa ukiifuatilia vizuri inavutia, lakini pia utaalamu wenu ni wa tofauti na sayansi nyingine, hivyo niwapongeze kwa kazi nzuri ya utabiri”. Alisisitiza Bw. Mchatta.
Kupitia maonesho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu “Tambua Soko, ongeza tija, tekeleza Dira 2050”, wageni wameendelea kupokea elimu mbalimbali ya hali ya hewa na kufahamu njia za usambazaji wa taarifa za Mamlaka, iliyopelekea wadau kuendelea kusajiliwa kupitia mifumo mbalimbali ya Mamlaka ili kuweza kupokea taarifa za hali ya hewa kidigitali.
Mamlaka inaendelea kuwaalika wadau mbalimbali kuendelea kutembelea katika mabanda ya TMA yaliyopo katika viwanja vya maonesho ya NaneNane, ambapo Kitaifa yanafanyika katika mkoa wa Dodoma na Kikanda ni katika mikoa ya Mbeya na Morogoro.

