Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Wajumbe wa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria katika Matukio ya Ghasia wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025 mara baada ya uzinduzi wa Tume hiyo, Ikulu, Jijini Dar es Salaam, tarehe 07 Agosti, 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Idd Azan Zungu wakishiriki katika hafla ya uzinduzi wa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria katika Matukio ya Ghasia wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 Ikulu, Jijini Dar es Salaam, tarehe 07 Agosti, 2026.