Timu ya taifa ya Paraguay imefanikiwa kuitoa Ujerumani katika mashindano ya Kombe la Dunia baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalti 4-3, kufuatia sare ya 1-1 iliyodumu kwa dakika 120 katika mchezo wa hatua ya 32 bora.

Kwa matokeo hayo, Paraguay imetinga hatua ya 16 bora kwa mara ya tano katika historia yake. Ushindi huo pia umeonekana kuwa kisasi kitamu baada ya kusubiri kwa miaka 24.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2002, nchini Korea Kusini na Japan, Ujerumani iliiondoa Paraguay katika hatua hiyo kwa ushindi wa bao 1-0, lililofungwa mwishoni mwa mchezo na Oliver Neuville. Safari hii, hata hivyo, Paraguay imeandika historia mpya kwa kuiondoa Ujerumani na kufuzu hatua inayofuata.