Naibu Katibu Mkuu Uwekezaji, Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu akipata maelezo kutoka kwa Mwanasheria George Mhina Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mkoani Geita.
Naibu Katibu Mkuu Uwekezaji, Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu akitoa maagizo kwa Mwanasheria George Mhina Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mkoani Geita.
Mwanasheria George Mhina Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa akifafanua jambo Kwa Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ali Gugu hayupo pichani wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mkoani Geita, Kulia ni Tobietha Makafu Afisa Uhusiano EWURA, Jesca Sewando Afisa Mwandamizi Huduma Kwa wateja EWURA na kushoto ni Lucy Michael Mhandisi wa Umeme EWURA.
Naibu Katibu Mkuu Uwekezaji, Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu akiondoka kwenye banda la EWURA mara baada ya kutembelea katika banda hilo huku akiwa ameongozana na Pellagy Richard Marando Afisa Mhifadhi Mwandamizi Hifadhi ya Taifa ya Gombe wakati akielekea kwenye banda la Maliasili kwenye maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mkoani Geita.
……………………………….
Mamlaka ya Kusimamia Nishati na Maji nchini (EWURA) imewataka washiriki mbalimbali katika maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanaofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili Mkoani Geita kutembelea banda la EWURA kwa lengo la kupata elimu juu ya huduma wanazozitoa.
Rai hiyo imetolewa na Mwanasheria Msomi Meneja wa Ewura kanda ya ziwa Mhandisi George Mhina alipokuwa akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Ally Gugu alipotembele banda la EWURA katika maonesho ya 5 hayo ya teknolojia ya madini yanayofanyika Mkoani Geita.
Mwanasheria George amesema EWURA inatoa huduma mbalimbali ikiwemo utoaji wa leseni katika vituo mbalimbali nchini vya kuuzia mafuta pamoja na kupanga bei za mafuta pamoja na maji pia wanaendelea kusimamia huduma ya mafuta nchi nzima ambapo wanaendelea kuratibu uwekezaji wa vituo vya mafuta maeneo ya vijijini ili kuimarisha uhakika wa huduma hiyo nchini.
Aidha amesema EWURA inasimamia utekelezaji wa mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi Tanzania unaotambulika kama (EACOP) na kwamba tayari tathimini ya athari ya kimazingira na kijamii ya Mradi huo zimeshafanyika, na wamejipanga kukabiliana nazo.
Ameongeza kuwa EWURA Imefanya vyema upembuzi na kujiridhisha kuwa mradi wa Bomba la Mafuta ni salama kwa mazingira na jamii hivYo watanzania waondoe shaka kwani mradi utatekelezwa kwa kuzingatia sheria na kanuni za kimazingira.
“Baadhi ya maeneo watu tayari wameshalipwa fidia, sasa hivi inajengwa kambi kubwa pale Nzega, ambapo mabomba yote yatakuwa yanawekwa pale na yanapakwa rangi pale baadaye yanasafirishwa kwenda sehemu zingine.”
“Tumepita kwenye vijiji vyote vya mkoa wa Geita na mkoa wa Kagera vijiji vyote ambapo huu mradi utapita, tumejiridhisha tunahamasisha kama mtu anafuga, afuge kweli kambi itakapojengwa huduma ya chakula ipatikane.” Amesema Mwanasheria George.