Home Biashara NAIBU KATIBU MKUU UWEKEZAJI WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA AKIWA KATIKA KLINIKI...

NAIBU KATIBU MKUU UWEKEZAJI WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA AKIWA KATIKA KLINIKI YA BIASHARA MAONESHO YA MADINI GEITA

0

Naibu Katibu Mkuu Uwekezaji, Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu akiwa katika banda la Kliniki ya Biashara lililoshirikisha taasisi wezeshi za Serikali ikiwemo Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ambapo alipata maelezo kutoka kwa mkuu wa banda hilo kutoka Mamlaka la Maendeleo ya Bishara TanTrade Bw. Petro Matulanya (kushoto), kuhusu utendaji wa taasisi hizo katika maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika eneo la Bomba mbili mkoani Geita.

Naibu Katibu Mkuu huyo alifanya ziara hiyo leo Octoba 4,2022 katika Maonesho hayo yanayofanyika katika uwanja wa EPZA maarufu Bomba mbili Mkoani Geita ambapo BRELA ni kati ya Taasisi zinazoshiriki katika Kliniki hiyo kusikiliza na kutatua changamoto za wadau na wananchi mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano (BRELA) Roida Andusamile (mwenye fulana ya Bluu) akifuatilia mazungo ya Mkuu wa Banda wa Kliniki ya Biashara katika Maonesho hayo ambaye ni Afisa Biashara wa TANTRADE Petro Matulanya (mwenye fulana nyeusi) alipokuwa akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Uwekezaji Ally Gugu (Hayumo pichani) wakati wa ziara fupi ya Kiongozi huyo katika Kliniki hiyo aliyoifanya leo Octoba 4,2022 Geita.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano (BRELA) Roida Andusamile akiendelea na kazi katika banda la BRELA.

Wafanyakazi wa BRELA wakiendelea na kazi katika banda hilo.