Home Mchanganyiko ASKOFU MCHAMUNGU AWATAKA WAKRISTO KUISHI MAISHA YA MTAKATIFU VINSENTI WA PAULO.

ASKOFU MCHAMUNGU AWATAKA WAKRISTO KUISHI MAISHA YA MTAKATIFU VINSENTI WA PAULO.

0

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la DSM, Askofu Henry Mchamungu akimlisha mtoto anayeishi katika mazingira magumu katika haflla ya kusherekea somo wa Mtakatifu Vinsenti wa PauloAskofu wa Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Henry Mchamungu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Mtakatifu Vinsenti wa Paulo.

……,…………………….

NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.

Wakristo nchini wametakiwa kuwa na upendo wa kweli katika maisha yao kwa kuonesha imani zao kwa njia ya matendo hasa katika kuhakikisha wanawasaidia watu wenye shida mbalimbali jambo ambalo litawasaidia kufikia ufalme wa Mbinguni.

Akizungumza katika Misa Maalamu ya Kusherekea somo wa Mtakatifu Vinsenti wa Paulo iliyofanyika hivi karibuni katika Parokia Ya Familia Takatifu Mburahati, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Askofu Henry Mchamungu, amesema kuwa katika maisha yetu ya hapa Duniani tunapaswa kujiweka katika nafasi ya watu wenye uhitaji ili tuone umuhimu wa kuwasidia.

Askofu Mchamungu amesema kuwa imani pasipo matendo ni sawa na bure, hivyo kila mkristo anakila sababu ya kuyaisha maisha ya Mtakatifu Vinsenti wa Paulo hasa katika kukaa katika nafasi ya watu mwenye uhitaji na kuwasaidia.

“Mtu mwenye thamani mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule anayewasaidia watu wenye shida, asiyekuwa na nguo apewe nguo, asiyekuwa na chakula apewe chakula, muhitaji anatakiwa kujaliwa, ukifanya hivyo utakuwa umefanya kitu cha maana” amesema Askofu Mchamungu.

Amesema kuwa Shirika la Mtakatifu Vinsenti wa Paulo wanajitaidi kuangaika na maisha ya watu katika kuhakikisha wanaendelea kutatua changamoto zilizopo kwa wahitaji hasa maskini na watu wasiojiweza kiuchumi.

Amesema kuwa imani za wakristo zinatakiwa kuonekana kupitia matendo yao jambo ambalo litawasaidia kuwa na nguvu ya kuendelea kuwasaidia waitaji.

Siku za mwisho watu watabaguliwa katika makundi mawili kama mchungaji anavyobagua mifugo yake, Mbuzi kulia na kondoo kushoto, wale waliotenda mema wataambiwa karibuni katika ufalme ulioandaliwa tangu zamani, kundi lengine ni wale ambao wamelaaniwa ambao hawajaguswa na waitaji katika maisha yao” amesema Askofu Mchamungu.

Askofu Mchamungu amefafanua kuwa huwezi kumsaidia kila mtu mwenye shida ila tunatakiwa kusaidia kadri ya uwezo wako Mwenyezi Mungu alivyokubariki.

Ameeleza kuwa maisha ya Mtakatifu Vinsenti wa Paulo alipokuwa mtoto kazi yake ilikuwa kuchunga mifugo na maisha ya watu wengi yalikuwa duni nchini Ufaransa alipokuwa akiishi na wazazi wake.

Amesema kuwa njiani wakati anakwenda kuchunga mifugo alikuwa akikutana na maskini, na aliguswa na kuwasaidia kwa chochote alichokuwa amebeba katika mfuko.

Ameeleza kuwa Baba yake baada ya kuona mtoto wake ana huruma ya kuwasaidia maskini, akaona amsaidie kwa kumbadilishia kazi yake ili baadaye awe katika nafasi nzuri ya kuwasaidia maskini.

Amesema kuwa Mtakatifu Vinsenti wa Paulo aliacha kazi ya kuchunga mifugo na kwenda kusoma kuwa Padri ili aweze kuwasaidia waitaji.

Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Mtakatifu Vinsenti wa Paulo, Bw. Vicent Kasambala, amesema kuwa utume wa shirika hilo wanafanya katika jumuia na jamii kwa jumla hasa katika kuwasaidia watu wenye shida mbalimbali shida ikiwemo wafungwa, maskini na wagonjwa.

Bw. Kasambala amefafanua kuwa Shirika la Mtakatifu Vinsenti wa Paulo wamendelea kufanya utume wao kwa kushirikiana na vituo mbalimbali vya kulea makundi maalamu ikiwemo watoto yatima, wazee na watu wenye uitaji kwa kuwasaidia maitaji yao.

Amesema kuwa katika kusherekea somo wa mtakatifu vinsenti wametoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo vya Mburahati, kijiji cha Msimbazi pamoja na kituo cha Kulea Watoto Yatima kilichopo Tabata.

Amebainisha kuwa Shirika la Mtakatifu Vinsenti wa Paulo lipo katika mpango wa kuwapatia bima ya afya watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa ambapo watakuwa wanapa huduma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa wana changamoto ya kupata matibabu ya afya, hivyo tumepanga kuwakatia bima ya afya ili waweze kupatiwa matibabu vizuri” amesema Bw. Kasambala.

Bw. Kasambala amefafanua kuwa katika kuhakikisha injili inasonga mbele wanatarajia kwenda, Wilaya ya Kibiti, Utete, Mafia kwa ajili ya kuwapatia msaada ya mifuko 100 ya saruji kufanikisha ujenzi wa  kanisa.

“Lengo kubwa ni kuendelea kuyaishi maisha ya Mtakatifu  Vinsenti wa Paulo kwa vitendo kama maandiko matakatifu yanavyosema tuwasaidie watu wenye uitaji katika maisha yetu ya hapa duniani” amesema Bw. Kasambala.     

Bi. Flora Alphonce kutoka Kituo cha Mburahati amelishukuru Shirika la Mtakatifu Vinsenti wa Paulo kwa kuendelea kuwasaidia na kuwataka watu wengine kuendelea kuwashika mkono katika shida zao.