Home Mchanganyiko TBL Plc yatoa msaada wa tani 10 za unga wa mahindi kwa...

TBL Plc yatoa msaada wa tani 10 za unga wa mahindi kwa wahanga wa mafuriko mkoani Kilimanjaro

0

Mkurugenzi wa Mauzo wa TBL wa kanda ya Kaskazini,James Bokella akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mh.Anna Mghwira, katika hafla hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mh.Anna Mghwira akipokea sehemu ya Masada wa unga wa mahindi uliotolewa na kampuni ya TBL kutoka kwa Mkurugenzi wa Mauzo wa kanda ya Kaskazini James Bokella,(kulia) aliyesimama kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa huo,Dk.Kazungu. 

………………………………………………..

Kampuni ya Tanzania Breweries Public Limited Company, imetoa msaada wa tani 10 za  unga wa mahindi  kwa wahanga wa mafuriko ya mvua kubwa iliyonyesha  mkoani Kilimanjaro  hivi karibuni.

Msaada huo  umekabidhiwa kwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa , Anna Mghwira, kwa ajili ya kuwapatia unafuu wa maisha  wakazi hao ambao nyumba zao ,mali zao na mashamba yaliharibiwa na  mvua hizo

Akiongea katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika mjini Moshi,Mkurugenzi wa Biashara wa TBL wa kanda ya Kaskazini,James Bokella,  alisema “Sisi kama TBL Plc tumejitoa kusaidia jamii tunayofanyia biashara zetu na hii ni moja ya njia yetu mojawapo ya kurudisha tunachokipata kwao hususani kipindi ambacho wanahitaji msaada.”

Kwa upande wake,Mheshimiwa  Anna Mghwira,    alitoa shukrani kwa msaada huo kutoka kampuni hiyo na  kutoa wito kwa taasisi nyinginezo na watu binafsi kusaidia wahanga hao wa mafuriko kulingana na uwezo wao.
TBL Plc, hivi karibuni  pia ilitoa msaada wa tani 9 za unga wa mahindi kwa wahanga wa mafuriko wa Rufiji mkoani Pwani.