Mkurugenzi wa Mauzo wa TBL wa kanda ya Kaskazini,James Bokella akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mh.Anna Mghwira, katika hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mh.Anna Mghwira akipokea sehemu ya Masada wa unga wa mahindi uliotolewa na kampuni ya TBL kutoka kwa Mkurugenzi wa Mauzo wa kanda ya Kaskazini James Bokella,(kulia) aliyesimama kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa huo,Dk.Kazungu.
………………………………………………..
Kampuni ya Tanzania Breweries Public Limited Company, imetoa msaada wa tani 10 za unga wa mahindi kwa wahanga wa mafuriko ya mvua kubwa iliyonyesha mkoani Kilimanjaro hivi karibuni.
Msaada huo umekabidhiwa kwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa , Anna Mghwira, kwa ajili ya kuwapatia unafuu wa maisha wakazi hao ambao nyumba zao ,mali zao na mashamba yaliharibiwa na mvua hizo
Akiongea katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika mjini Moshi,Mkurugenzi wa Biashara wa TBL wa kanda ya Kaskazini,James Bokella, alisema “Sisi kama TBL Plc tumejitoa kusaidia jamii tunayofanyia biashara zetu na hii ni moja ya njia yetu mojawapo ya kurudisha tunachokipata kwao hususani kipindi ambacho wanahitaji msaada.”