Home Mchanganyiko Rais Mhe. Magufuli akutana na Rais Shein, Mzee Mangula na Dkt. Bashiru,...

Rais Mhe. Magufuli akutana na Rais Shein, Mzee Mangula na Dkt. Bashiru, Ikulu Chamwino

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Juni, 2020 amekutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein katika kikao cha ndani kilichofanyika Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mhe. Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.
Mohamed Ali Shein, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi Mzee Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM
Dkt. Bashiru Ally Kakurwa wakifuraia jambo leo tarehe 03-
06-2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi-Bara Mzee Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru  Ally Kakurwa wakiwa katika kikao cha ndani  leo tarehe 03-06-2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein akiangalia
akiweka udongo katika jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za Ikulu na kukagua maendeleo ya kazi ya ujenzi wa ofisi hizo inayofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia shirika lake la Suma JKT.

Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein akiangalia kibao cha jiwe la msingi la Ujenzi wa Uwekaji Ofisi za Ikulu ya Chamwino.

Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein
akizungumza na wajenzi kutoka JKT mara baada ya kukagua kazi za Ujenzi wa Ofisi za IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein Ikulu ya Chamwino Dodoma leo.

PICHA NA IKULU