Home Mchanganyiko MHE.UMMY AMEUPATIA  UONGOZI WA MKOA WA SINGIDA MIEZI SITA KUKAMILISHA VYUMBA VYA...

MHE.UMMY AMEUPATIA  UONGOZI WA MKOA WA SINGIDA MIEZI SITA KUKAMILISHA VYUMBA VYA HOSPITALI 

0

*****************************

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameupa uongozi wa Mkoa wa Singida miezi sita kuhakikisha unasimamia ujenzi wa jengo lenye vyumba vya Radiolojia, Maabara, Chumba cha upasuaji na Wodi ili uweze kukamilika na kuanza kutoa huduma ifikapo terehe 30 Disemba mwaka huu.

Waziri Ummy ametoa wito huo mapema leo wakati alipotembelea ujenzi wa jengo hilo ambalo bado lipo katika hatua ya msingi linalopatikana katika Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Singida. “Wizara imetoa Tsh. Bilioni 2.5 kwa ajili ya ujenzi wa jengo hili muhimu ambalo litasaidia Wananchi wa Singida kupata huduma bora za kibingwa, hivyo ninatoa miezi sita kuanzia leo liwe limeshakamilika na kuanza kutoa huduma ifikapo tarehe 30 Disemba 2020”. Amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy ameutaka uongozi wa Manispaa ya Singida kuharakisha kuhamisha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya sasa kupeleka huduma katika Hospitali mpya ya Rufaa ya mkoa iliyojengwa eneo la Mandewa na kuanza kutoa huduma kuanzia tarehe 1 Januari 2021.
Pia ameitaka Hospitali hiyo kurudishwa kwa manispaa ili itumike kama Hospitali ya Manispaa mara baada ya huduma za rufaa kuhama.

Kabla ya kuhitimisha ziara yake Mkoani Singida Waziri Ummy ametembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali ya sasa Rufaa ya Mkoa huo na kuongea na baadhi ya wagonjwa na watumishi na baadae kuelekea Mandewa ambapo Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa inajengwa na kukagua baadhi ya maeneo na kuongea na baadhi ya watumishi na wagonjwa waliofika kupata huduma