Maonyessho ya Nne ya bidhaa za viwandani yamefikia tamati leo tarehe 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Mwl. J.K Nyerere (Sabasaba). Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeshiriki katika Maonyesho hayo. Wakati akifunga maonyesho hayo Mgeni rasmi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bwana Leo Lyayuka amesema kuwa Maonyesho hayo yamekuwa chachu ya maendeleo katika kufikia uchumi wa kati wa maendeleo ya Viwanda huku akiwataka wadau wote wa Viwanda na Biashara Kupanua wigo wa Biashara kwa Maendeleo ya Nchi yetu.
Mgeni rasmi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bwana Leo Lyayuka (Kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Tantrade Bwana Edwin Rutageruka.
Mgeni rasmi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bwana Leo Lyayuka amekabidhi cheti cha ushiriki kwa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na kupokelewa na Bi Robertha Makinda, Afisa Habari na Mawasiliano BRELA.
Wafanyakazi wa BRELA wakiwa kwenye banda la Maonyesho ya Bidhaa za Viwanda katika uwanja wa Mwl. J.K Nyerere ( Sabasaba) kutoka kulia ni Hilary Mwenda Afisa Tehama, Robertha Makinda Afisa Habari na Mawasiliano,Yusuph Nakapala Afisa Leseni, Ruth Mmbaga Afisa Mwandamizi Msaidizi wa Usajili na Hellen Mhina Msaidizi wa Usajili Mkuu.
Wateja mbalimbali waliotembelea banda la BRELA na kupatiwa Elimu ya kurasimisha biashara zao.