Home Biashara Benki ya NMB yatwaa Tuzo ya NBAA kwa mwaka mwingine mfululizo

Benki ya NMB yatwaa Tuzo ya NBAA kwa mwaka mwingine mfululizo

0

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaabani, akimkabidhi Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa, Tuzo ya Benki Bora katika utayarishaji wa ripoti za kifedha kwa mwaka 2019, iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NBAA). Hafla ya kukabidhiwa tuzo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. (Na Mpiga Picha Wetu).

Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa, akionesha Tuzo aliyoipokea ya Benki ya NMB kuwa Benki Bora katika utayarishaji wa ripoti za kifedha kwa mwaka 2018, iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).

Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa utoaji tuzo.

……………………………………………….

BENKI ya NMB imetwaa tuzo maalum kutoka Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu(NBAA) kama Benki bora ya Taarifa za Kifedha zilizokaguliwa na kutambuliwa kimataifa kwa mwaka 2018,ilikoshinda benki kadhaa nchini.

Benki hiyo imetambuliwa kwa kufikia kiwango bora katika utayarishaji wa taarifa zake za kifedha, kulingana na mahitaji ya taarifa (viwango vya kuripoti za kitaifa na kimataifa).

Hafla ya kukabidhiwa tuzo hiyo ambayo kwa NMB, ni ushindi wa mara ya pili mfululizo, ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ambapo NBAA ilisema taarifa za mahesabu za NMB zimeendelea kuwa bora kila mwaka, ubora uliowasukuma majaji kuwapa tuzo hiyo kwa mara nyingine.

Akizungumzia vigezo vilivyotumika kupata washindi, Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA Mr.Pius Maneno, amesema walipatikana kwa kuangalia washiriki waliovuka asilimia 75 ya vigezo vilivyowekwa.

Naye Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Mr. Benedicto Baragomwa, amesema wao kama wataalam wa masuala ya fedha, wanatambua umuhimu wa kuandaa vitabu vya mahesabu vya Benki kwa njia na mifumo inayozingatia viwango vya kitaifa na kimataifa.

“Ushindi huu unadhihirisha namna ambavyo tumejikita katika kudumisha uadilifu wa hali ya juu kwenye uwasilishaji wa taarifa zetu za kifedha za mwaka,” alisema Baragomwa baada ya kupokea tuzo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani.

Baragomwa alibainisha kuwa, wawezeshaji wa benki hiyo wameandaliwa katika misingi inayofuata na kuheshimu viwango vya kimataifa vinavyotambuliwa na IFRS, pamoja na mahitaji ya ndani.

Taarifa iliyotolewa na Benki hiyo imetoa shukrani kwa wafanyakazi na kujivunia mfumo bora wa Uongozi na utendaji hasa kitengo cha fedha. “Tuzo hii imepatikana nyuma ya mfumo uliopo wa utawala bora na michakato ya udhibiti ambayo inakuza uwazi wa taarifa za kifedha, uwajibikaji,ueledi na kiwango cha juu cha uadilifu wa takwimu. Hongera kwa kila mtu, haswa timu ya kifedha kwa kuongoza maandalizi ya Taarifa ya Fedha ya Benki ya NMB.

#NMBKaribuYako