Home Mchanganyiko VETA INAWAJENGEA MAZINGIRA MAZURI VIJANA KUJIAJIRI

VETA INAWAJENGEA MAZINGIRA MAZURI VIJANA KUJIAJIRI

0

*********************************

NA EMMANUEL MBATILO

Wahitimu wa Chuo cha Ufundi VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam wamewataka vijana kujiunga na VETA ili kuweza kupata mafunzo mbalimbali ambayo yatamuwezesha kujijengea kujiajili na kuacha kutegemea kuajiriwa.

Akizungumza katika maonesho ya Viwanda vya Biashara katika Viwanja vya maonesho vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam,mmoja wa Wahitimu wa Chuo cha Ufundi VETA, Bw.Zadock James ameshukuru uongozi wa VETA kwa kuwapatia vifaa kwaajili ya kukuza na kuendeleza ujuzi walionao ambao unawasaidia kujiwekea mazingira mazuri ya kujiajiri.

“Tumeamua kujikusanya kikundi na kuamua kujiajili katika ufundi Seremala na tunaishukuru VETA kwa kutupatia ushirikiano wa kutosha kwa kutuamini na kutupatia vifaa bure kwaajiri ya kukuza ujuzi wetu”.Amesema Bw.James.

Pamoja na hayo Bw.James ametoa wito kwa vijana kuwa waweze kuwa na udhubutu wa kujijengea utamaduni wa kujiajili ili kuondokana na vishawishi vya kujiingiza katika makundi mabaya.