Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), ashiriki Mkutano wa Masuala ya Amani, Usalama na Maendeleo ya Watu unaoendelea katika Jiji la Niamey nchini Niger. Mkutano huo wa siku tatu ambao umeandaliwa na Shirika la Universal Peace Federation, umewaleta pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali, Maspika, Manaibu Spika, Mawaziri, Wabunge, Viongozi wa Dini na Kimila pamoja na Wakuu wa Taasisi za Kibiashara wa Bara la Afrika kubaini na kujadili changamoto zinazosababisha uvunjifu wa amani na usalama katika kuwaletea maendeleo Waafrika. Katika Mkutano huo Naibu Spika ameambatana na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Zainabu Katimba.