Bw. Jianpo Zhang akiwa na mkewe Shamsa Shaban Zhang wakiwa katika hafla hiyo wakifurahia pamoja na wageni waalikwa mbalimbali.
Bw. Jianpo Zhang akiwa na mkewe Shamsa Shaban Zhang wakiwa katika hafla hiyo wakifurahia pamoja na wageni waalikwa mbalimbali wakipata burudani ya muziki.
Baadhi ya wageni mbalimbali walioshiriki katika hafla hiyo ya kuwapongeza.
……………………………………………
MWANAFUNZI wa Chuo cha Mzumbe ambaye ni raia kutoka China Jianpo Zhang amesema anajisikia fahari kuoa Tanzania akidai kufanya hivyo mbali na kudumisha undugu baina ya familia hizo pia kunazidi kuboresha mahusiano baina ya Tanzania na China.
Aliyasema hayo wakati wa sherehe ya kuwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza kwa namna moja au nyingine kufanikisha harusi yake na mkewe Shamsa Shaban Zhang iliyofanyika wiki iliyofanyika Jijini Dar es Salaam juzi na kuudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mkuu wa Majeshi mstaafu Robert Mboma.
Zhang alisema anajivunia kuoa mtanzania huyo akisisitiza kuwa binadamu wote ni ndugu na kwamba kitendo chake cha kufunga ndoa hiyo kitazidi kumfanya ajisikie kuwa kama yupo nyumbani huku akiwataka watanzania kuona fahari pia kwenda kuoa raia kutoka China.
Alisema katika kipindi cha miaka mitatu aliyoishi hapa nchini ameona mambo mengi mazuri na kiasi cha kumfanya ajihisi yupo ‘nyumbani’ na zaidi akidai kuwa amani na upendo kutoka kwa watanzani ndiyo hasa jambo linalozidi kumuongezea hamasa ya kuona undugu unazidi kukua baina ya mataifa yote mawili.
Alisema furaha kwake Tanzania inazidi kukua kimaendeleo siku hadi siku chini ya uongozi wa Rais John Magufuli ambaye pia anasema katika utawala wake ameona wazi wazi ushirikiano baina ya Tanzania na China ukizidi kuhimarika.
“Naipenda Tanzania, nawapenda watu wake na zaidi Rais John Magufuli ambaye katika utawala wake naona mambo mengi mazuri ukiwemo ujenzi wa miradi mbalimbali ikifanyika katika kiwango cha hali ya juu” alisema Zhang.
Alisema mipango yake ya baadae ni kufanya biashara mbalimbali zinazoakisi mahitaji uhimu ya kijamii ili ziweze kuzidi kumuweka karibu na watanzania anaodai kuwa kwa sasa ni ndugu zake hasa baada ya kumuoa mtanzania.