Home Mchanganyiko MKUU WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI – CGP PHAUSTINE KASIKE AANZA ZIARA...

MKUU WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI – CGP PHAUSTINE KASIKE AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MANYARA

0

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini – CGP Phaustine Kasike (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Lipina Lyimo(katikati) pamoja na Kamishna Msaidizi wa Magereza, Masoud Kimolo(kulia) muda mfupi alipowasili leo Novemba 16, 2019 Mkoani humo. CGP Kasike yupo mkoani Manyara kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua magereza yote ya Mkoa huo na kuzungumza na Maafisa na askari wa Jeshi hilo.

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini – CGP Phaustine Kasike(meza kuu) akiongoza
kikao kazi na Maafisa wa Magereza Mkoani Manyara kabla ya kufanya Baraza la Wafungwa na mahabusu wa Gereza Babati.

Mkuu wa Magereza Mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Anderson
Kamtiaro(kulia) akimuonesha Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini – CGP Phaustine
Kasike(kushoto) shamba la maharage ambalo limelimwa kwa kutumia Kilimo cha umwagiliaji Gereza Arusha.

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini – CGP Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Magereza Mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Anderson Kamtiaro(kulia)alipokagua Shamba la mahindi kabla ya kuendelea na ziara ya kikazi Mkoani Manyara leo Novemba 16, 2019(Picha zote na Jeshi la Magereza).

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini – CGP Phaustine Kasike akisalimiana na Maafisa wa Magereza Mkoani Manyara mara baada ya kuwasili Gereza Babati kwa ziara yake ya kikazi leo Novemba 16, 2019.