Home Mchanganyiko TISER WAJA NA MWAROBAINI WA MIGOGORO YA ARDHI MVOMERO

TISER WAJA NA MWAROBAINI WA MIGOGORO YA ARDHI MVOMERO

0

Picha ya pamoja baada ya kumaliza semina iliyowakutanisha wajumbe wa
balaza la ardhi kata ya Dakawa, na wasuruhishi wa mabalaza ya ardhi.

Mkurugenzi wa taasisi ya Tanzania initiative for social and economic relief
( TISER) Otana Nicholus akisalimia na mzee Bwana Philipo Kipuyo mjumbe wa
balaza la wasuruhishi kata ya Dakawa.

****************************************

NA FARIDA SAIDY, MOROGORO

Licha ya Rais wa jamuhuri ya mungano wa Tanzania Dk Jonh Pombe Magufuli
kumuagiza mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Loata Ole Sanare kuhakikisha
anamaliza migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji katika mkoa wa
morogoro baada ya kuapishwa kuwa mkuu wa mkoa huo, lakini imeonekana
elimu ya matumizi bora ya ardhi ndio kikwazo kikubwa kwa wananchi.

Hayo yamebainika baada ya asasi isiyo ya kiserikali ya Tanzania initiative for
social and economic relief ( TISER) linashughurikia utatuzi wa migogoro ya ardhi
kati ya wakulima na wafugaji pamoja na jamii kwa ujmla, kufanya semina katika
kata ya Hembeti, Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, yenye lengo la kupeana
uzuefu wa utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Semina hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kata ya Hembeti,wajumbe wa balaza la ardhi kata ya Dakawa, wasuruhishi wa mabalaza ya ardhi kutoka katika kata hizo,pamoja na wawakirishi kutoka taasisi ya TISER.

Katika semina hiyo wasuruhishi wa mabalaza ya ardhi wamesema kuwa
wanaishukuru taasisi ya TISER kwa kuwapatia semina ambayo imewajengea
uwezo mkubwa katika kutatua migogoro ya ardhi katika vijiji vyao, kwani awali
hawakuwa na uwezo mkubwa katika utatuzi wa migogoro hiyo,hivyo wataenda
kufainyia kazi na wanaamini migogoro ya ardhi itaisha katika vijiji vyao.

Hata hivyo wameimba serikali kushirikiana na asasi mbalimbali katika
kuwaelimisha wananchi hususani wakulima na wafugaji juu ya athari za migogoro ya ardhi katika jamii.

Kwa upande wake Bwana Philipo Kipuyo mjumbe wa balaza la wasuruhishi kata
ya Dakawa lakini pia anatokea katika jamii ya wafugaji amesema kuwa TISER
imewasaidia kutatua migogoro ya ardhi katika kata hiyo,ambapo kwa sasa
wakulima na wafugaji wanakaa kwa amani na familia zao zinaweza
kuona(kuchumbiana baaina ya familia ya mkilima na mfugaji) na kuishi pamoja.

Aidha amesema kuwa mbinu zilizotumika katika kutatua migogoro hiyo ni pamoja na kuwakutaisha wakulima na wafugaji pale mgogoro unapotokea, jambo ambalo limesaidia kumaliza kabisa migogoro katika kijiji chao.

Nae mkurugenzi wa taasisi ya TISER bwana Otana Nicholus amesema kuwa mladi wa kutatua migogoro ya ardhi na kudumisha amani wilaya ya mvomro unalengo la kumaliza kabisa swala la migogoro ya ardhi katika wilaya ya mvomero.

Ambapo kwa sasa mladi huo unatekelezwa katika vijiji mbalimbali ikiwemo
milama,hembeti,dakwa sokoine, mpapa,ruhindo na mkambala,aidha amesema
TISER imeona mvomero kuna migogoro ndio maana wamejikita wilayani humo ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya migogoro ya ardhi.