Rodrygo akishangilia baada ya kutokea benchi na kuifungia Real Madrid bao la ushindi dakika ya 80 ikiwalaza Inter Milan 3-2 kwenye mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Alfredo Di Stefano Jijini Madrid. Real Madrid ilitangulia kwa mabao ya Karim Benzema dakika ya 25 na Sergio Ramos dakika ya 33, kabla ya Inter Milan kuzinduka kwa mabao ya Lautaro Martinez dakika ya 35 na Ivan Perisic dakika ya 68. Kwa ushindi huo, Real Madrid inafikisha pointi nne sawa na Shakhtar Donetsk, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi moja na BorussiaMönchengladbach, wakati Inter Milan inaendelea kushika mkia kwa pointi zake mbili baada ya kila timu kucheza mechi tatu PICHA ZAIDI SOMA HAPA
REAL MADRID YAFUFUKA LIGI YA MABINGWA YAITANDIKA 3-2 INTER MILAN
By Alex Sonna
November 4, 2020 | 8:20 am

Related Stories
View all
Michezo
11 hours ago
MAKAMU WA RAIS BALOZI DKT. NCHIMBI, ATEMBELEA UWANJA WA AFCON ARUSHA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Arusha,…
Michezo
3 days ago
ELLIOT ANDERSON ATUA MANCHESTER CITY KWA PAUNI MILIONI 116
Na. Fullshangwe Michezo, Updates Manchester, England – Manchester City imekamilisha usajili wa kiungo Elliot Anderson kwa dau linaloripotiwa kufikia pauni milioni 116, huku mchezaji…
