Na. Fullshangwe Michezo, Updates 

Manchester, England – Manchester City imekamilisha usajili wa kiungo Elliot Anderson kwa dau linaloripotiwa kufikia pauni milioni 116, huku mchezaji huyo akisaini mkataba wa miaka mitano utakaomuweka Etihad Stadium hadi mwaka 2031.Anderson, mwenye umri wa miaka 23, amejiunga na mabingwa hao wazamani wa Ligi Kuu England akitokea Nottingham Forest, ambako alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu kutokana na uwezo wake wa kutawala safu ya kiungo, ubunifu na kufanya kazi kubwa ndani ya uwanja.

Usajili huo unaonyesha dhamira ya Manchester City ya kuendelea kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya mashindano ya ndani na kimataifa msimu ujao.