Na Sixmund Begashe, Moshi

WAPENZI wa michezo wa Mkoa wa Kilimanjaro wameendelea kushuhudia Wizara ya Maliasili na Utalii ikisomba medali ya tatu ya dhahabu baada ya mkimbiaji wake Bi. Naomi Mgumba kuibuka mshindi tena kwenye mbio za Mita 150, kwenye Michezo ya SHIMIWI 2026.

Bi. Mgumba pia aliibuka mshindi wa mbio za Mita 1,500 akikimbia kwa dakika 5:48:99 huku nafasi ya pili ikichukuliwa na mkimbiaji wa Mahakama akimaliza kwa dakika 5: 59:61.

Mwenyekiti wa Club ya Maliasili Sports Club Bw. Elia Mtalemwa amesema kupitia ushindani mkubwa na ushindi walioupata wameweza kuitangaza vyema Wizara hiyo kupitia Club hiyo kwenye michezo hiyo yenye mvuto wa kipekee hapa nchini. 

Bw. Mtalemwa pamoja na kuushukuru uongozi wa Wizara, amewapongeza wachezaji wote kwa kuiheshimisha Wizara hiyo yenye inayochangia zaidi ya asilimia 2O katika pato la Taifa, huku akiwashukuru mashabiki wote wa Club hiyo waliojitokeza kwa wingi kutoka Arusha, Tanga na Mkoa wa Kilimanjaro ambao ndiyo wenyeji wa michuano.