Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliopigwa leo, Novemba 21, 2026, kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.
Mabao ya Simba yamefungwa na Elie Mpanzu pamoja na Libasse Guèye, wote wakitikisa nyavu kipindi cha kwanza katika mchezo wa raundi ya 11 ya ligi hiyo.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha pointi 33 na kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa imecheza mechi 11, sawa na Yanga SC, ambao wana pointi 28.
