Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa Chama hicho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kasulu mjini wilayani Kasulu wakati akiwa njiani kuelekea Kigoma mjini leo Alhamis Septemba 17, 2020.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-KASULU)
Baadhi ya wana CCM wakifurahia jambo wakati Rais Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na kuwaomba kura.
Mgombea ubunge jimbo la Kasulu Profesa Joyce Ndalichako akimuombea kura kwa wananchi wa Kasulu mjini wilayani Kasulu Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati akiwa njiani kuelekea Kigoma mjini leo Alhamis Septemba 17, 2020.
Sehemu ya maelfu ya wananchi waliojitokeza mjini Kasulu ili kumsikiliza mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Kasulu.