Home Siasa DKT.MWINYI KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA YA KUANZISHA VIWANDA KISIWANI PEMBA ENDAPO ATACHAGULIWA KUWA...

DKT.MWINYI KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA YA KUANZISHA VIWANDA KISIWANI PEMBA ENDAPO ATACHAGULIWA KUWA RAISI

0

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi, akizungumza na Wavuvi,Wakulima wa Mwani na Wafugaji wa Samaki katika hoteli ya Wesha Chake chake.

***************************************

NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi kuwa Rais atafanya mageuzi makubwa ya kuanzisha Viwanda kisiwani Pemba.

Alisema viwanda hivyo vitasaidia kuchakata na kusindika mazao ya baharini ili wavuvi na wakulima wa zao la mwani  wawanufaike.

Ahadi hiyo aliitoa wakati akizungumza na wakulima wa mwani,wavuvi na wafugaji samaki huko katika ukumbi wa mikutano katika Hoteli ya Wesha kisiwani humo.

Dk.Hussein, alisema dhamira yake ni kuhakikisha wananchi wa makundi yote wananufaika na rasilimali za nchi yao.

Alisema mazao ya baharini yakiwekewa miundombinu rafiki ya kiasasa ikiwemo kuanzishwa kwa viwanda vikubwa na vidogo, mazao hayo yataongezeka thamani na kuwanufaisha wamanchi wenyewe.

Aliongeza kuwa katika utawala wake ataweka ulinzi katika maeneo ya bahari kuu ili kuthibiti wizi wa samaki unaofanywa na meli kubwa katika maeneo ya bahari.

“Mkinichagua  kiukweli nina nia thabiti ya kuwatumikia wananchi  na kuyetekeleza kwa vitendo yote niliyowaahidi msiiwe na shaka juu ya hilo mnalolitegemea kutoka kwangu”alisema Dk Mwinyi.

Kwa Upande katibu wa jumuia ya wavuvi Pemba Khamis Sharif Haji amesema ilikufikia lengo la uchumi wa blue kwao nilazima wapatiwe mitaji na vitendea kazi vya kutosha na vyakisasa ambavyo vitawawezesha kufanya kazi zao kwa umahiri na kuweza kuleta tija.

“Mh : ili tufikiee huo uchumi blue ni lazima tupatiwe nyenzo za kisasa kwani uwezo wetu ni mdogo wengi wetu tunafanya  uvuvi wa kijadi hatutaki mameli maakubwa tupaatiwe japo mashua za mbao” amesema Dk: Husein.

Aidha Mgombea huyo wa urais Amezungumza na Waendesha bodaboda wa mkoa wa kusini Pemba ,na kuahidi kuimarisha kazi yao hiyo na kutambuliwa rasmi Serikalini .

Amesema changamoto zinazowakabili ya tozo kubwa la bima atalishughulikia kwa kukaa na vyombo husika ilikuona wanafanyakazi hiyo bila ya usumbufu .

Mapema Mgombea huyo wa Urais mara baada ya kuzungumza na wavuvi na wakulima hao, amewatembelea wafanya biashara,waendesha bodaboda,walimu pamoja na kuhudhuria kongamano la umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi na kuomba ridhaa ya kuweza kumchagua kuwa Rais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu utakao fanyika October 28, 2020.