Stella Kahwa Mkurugenzi wa Ufundi Wakala wa Vipimo (WMA) amesema Vipimo ni Viwanda na Viwanda ni Vipimo, Huwezi kuzalisha bidhaa yoyote bila vipimo vilivyothibitishwa ubora, Na ubora wa kitu lazima kuwe na kipimo ndiyo maana Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) ipo kwa ajili ya kazi hiyo
Stella Kahwa ameyasema hayo leo jijini Dar alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya vipimo duniani ambayo huadhimishwa Mei 20 kila mwaka.
Ameongeza kuwa wiki yote iliyopita maofisa wa taasisi hiyo walikuwa wakipita katika maeneo mbalimbali nchini kote ili kujiridhisha na kuwakumbusha wananchi kuhakikisha vipimo vyao vinakaguliwa na kuthibitishwa kwamba vina ubora katika upimaji wa bidhaa kwa ujumla.
Ametolea mfano kwamba na kusema “Vipimo ni muhimu kila mahali kwa mfano hospitali ile mizani inayotumiwa kupima uzito wa wagonjwa isipothibitishwa ubara wake daktari anaweza kumwandikia kipimo kikubwa kuzidi uzito wa mgonjwa jambo ambalo litamfanya mgonjwa huyo kushindwa kuhimili kwa sababu uzito wake utakuwa siyo sawa na kipimo ambacho mizani ilitoa majibu”. amesema.
Hivyo suala zima la vipimo ni muhimu katika kila sehemu, ili kupata Ujazo, uzito, Uwingi wa vitu, Urefu, Uzalishaji , Uuzaji, Manunuzi na kadhalika lazima utahitaji kutumia vipimo sahihi.
Mei 20 huadhimshwa kila mwaka kama siku maalum ya vipimo duniani ambayo iliasisiwa Mei 20 mwaka 1875 wakati makampuni kadhaa huko ufaransa yalipokutana na kujadili kuhusu vipimo hivyo, ambapo yalikipitisha kipimo cha ujazo wa Mita, Baada ya hapo tarehe hiyo iliteuliwa kuwa siku ya vipimo na imekuwa ikiadhimishwa duniani kote.