Home Michezo KEAN ATUPA DONGO KWA MASTAA WA KLABU YA MANCHESTER UNITED

KEAN ATUPA DONGO KWA MASTAA WA KLABU YA MANCHESTER UNITED

0

NA EMMANUEL MBATILO

Nahodha wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Roy Kean amewatupia lawama mastaa wa timu hiyo Rashford pamoja na Lingard akidai ni wachezaji ambao wanalipwa pesa ndefu na hawaonyeshi viwango vinavyolidhisha.

“Ukiangalia Matthijs de Ligt anaongoza Ajax akiwa na miaka 19 na analipwa pesa ya kawaida. Wakati huo Rashford anafunga bao 10 msimu mzima, free kicks zake zinaua mashabiki waliopo kwenye viti vya walemavu analipwa £100k & Lingard analipwa £120k kuwa mtu wa Instagram”. Amesema gwiji huyo.

Kean kwasasa ni kocha msaidizi wa klabu ya Nottingham Forest inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza maalufu kama Championship.