Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwa amenyanyua mkoba wa Bajeti Kuu ya Serikali, ya mwaka 2020/2021 bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha bungeni jijini Dodoma Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2020/2021.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akipongezwa na Wabunge baada ya kuwasilishwa Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2020/2021, bungeni jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, (wa tatu kushoto) na Wakuu wa Taasisi, Idara wa Wizara hiyo na Viongozi wengine wa Serikali wakisikiliza kwa makini hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya Sh. trilioni 34.9 kwa mwaka wa fedha 2020/2021, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2020/2021, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na Mkewe, Bi. Mbonimpaye Mpango wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula baada ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2020/2021, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa tatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara hiyo baada ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2020/2021, Bungeni jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)