Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe. Floribert Anzuluni Isiloketsh, ambaye ni Mjumbe Maalumu wa Rais wa DRC, Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, viongozi hao walijadili namna ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na DRC katika maeneo mbalimbali yenye maslahi ya pamoja, hususan biashara na uwekezaji, maendeleo ya miundombinu ya uchukuzi, kilimo, afya, ulinzi na usalama, pamoja na sekta ya madini.
Mazungumzo hayo yanaakisi dhamira ya Viongozi wa Wakuu wa nchi hizo mbili ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidugu na ushirikiano wa kimkakati kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

