YANGA SC  imeendelea kukusanya pointi ikishinda mechi ya nne mfululizo katika Ligi Kuu Bara, baada ya leo Agosti 28, 2026 kuichapa Pamba Jiji mabao 2-0.

Ushindi huo unairudisha Yanga juu ya msimamo wa ligi, ikifikisha pointi 12 sawa na Simba, lakini bingwa mtetezi akibebwa na tofauti nzuri ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Dakika 17 tu zilitosha kwa Yanga kupata bao la kuongoza likifungwa na Maxi Nzengeli, akiitumia asisti ya mshambuliaji, Cheikh Toure. Wakati Pamba Jiji ikijiuliza, ikaruhusu bao lingine dakika ya 22 mfungaji akiwa Toure akimalizia pasi ya Peter Shalulile.