Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo, Agosti 27, 2026, katika Uwanja wa Major General Isamuhyo uliopo Mbweni, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, Simba SC imefikisha pointi 12 na kuongoza Ligi Kuu Tanzania Bara. Wapinzani wao, Yanga SC, wana pointi 9 baada ya kucheza michezo mitatu, huku Simba SC ikiwa imecheza michezo minne.