NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
CHUO cha Usimamizi wa Fedha (IFM), kimesema elimu ya juu haipaswi kuishia kumpa kijana cheti, bali kumjengea uwezo wa kutumia maarifa na ujuzi kujiajiri, kuzalisha ajira na kutatua changamoto zinazoikabili jamii.
Akizungumza jana (Jumamosi) katika banda la chuo hicho kwenye Maonesho ya Nane Nane, Kanda ya Ziwa Magharibi, Mkuu wa Utawala wa IFM, Kampasi ya Mwanza, Dr. Lawrence Sunga Joseph, alisema chuo hicho kimeweka mkazo katika kuwajengea wanafunzi uwezo wa ubunifu na ujasiriamali sambamba na taaluma wanazosoma.
“Chuo cha IFM kimejikita katika ufundishaji, utafiti na ushauri wa kitaalamu, kinatoa programu za diploma, shahada za kwanza na za uzamili. Kinataka wanafunzi wake wahitimu wakiwa na uwezo wa kutumia taaluma zao katika mazingira halisi ya kazi, biashara na uzalishaji, badala ya kutegemea ajira za kuajiriwa pekee.” alisema Dk. Sunga .
Alisema wanafunzi chuoni mbali na masomo ya taaluma hufundishwa pia, ujuzi na ubunifu unaowawezesha kubuni bidhaa na huduma zinazoweza kutatua changamoto za jamii, huku baadhi yao wakifanikiwa kuanzisha shughuli za uzalishaji, zikiwemo bidhaa za mapambo ya ndani, mafuta ya kupaka na vifaa mbalimbali.
Kwa mujibu wa Dr. Sunga, ubunifu uliofanywa na wanafunzi ni jiko linalotumia mafuta machafu lta moja kwa siku, limelenga kutumia nishati hiyo kwa ufanisi huku likisaidia katika utunzaji wa mazingira, likiwa mfano wa namna elimu ya ubunifu inavyoweza kugeuza changamoto za mazingira kuwa fursa za kiteknolojia na kiuchumi.
“Tunawafundisha wapate skills (ujuzi) na ubunifu kwa mwanafunzi kutengeneze kitu ( bidhaa) kwa kutumia malighafi zilizopo. Tunatoa elimu ya competence ili mwanafunzi atoke akiwa na skills za maisha, aweze kutengeneza bidhaa za kusaidia watu,” alisema Mkuu huyo wa Utawala.
Aliongeza kuwa wanafunzi hupewa assignments zinazowataka kubuni vitu mbalimbali, huku baadhi yao wakifanikiwa kutengeneza programu za kompyuta za kusaidia kufanya hesabu (stocktaking), hatua inayowajengea uwezo wa kutumia teknolojia kutatua changamoto za biashara.
Dr. Sunga alisema mfumo huo wa elimu unalenga kuhakikisha mhitimu anatoka chuoni akiwa na zaidi ya cheti cha kitaaluma, kwani anapaswa kuwa na uwezo wa kutumia maarifa yake katika kujiajiri na kutoa huduma kwa jamii.
Hivyo, kwa mantiki hiyo, IFM imeendelea kuunganisha mafunzo ya darasani na ujuzi wa vitendo, ubunifu na ujasiriamali ili kuwasaidia vijana kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto ya ajira nchini.
“Fursa hizo zinaendana na mahitaji ya dunia ya sasa ambayo inazidi kutegemea teknolojia katika uzalishaji, biashara, huduma za fedha na mawasiliano. Programu hizi zinaongeza wigo wa taaluma zinazopatikana chuoni, sambamba na dhamira ya taasisi ni kutoa elimu inayokidhi mahitaji ya jamii na soko la ajira,” alisema Dr.Sunga.
Aidha, taaluma hizo ni muhimu katika kujenga wataalamu wenye uwezo ili kukidhi mahtaji ya soko na kufanya uchambuzi wa hatari, kusimamia masuala ya fedha, uhasibu, uchumi, benki, bima , teknolojia, usimamizi wa kodi na kutumia takwimu na maarifa ya kifedha katika kufanya maamuzi ya kitaalamu.