Timu ya Taifa ya Argentina imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuichapa Misri mabao 3-2 katika mchezo wa hatua ya 16 bora wa Kombe la Dunia 2026.
Kwa matokeo hayo, Misri imeaga mashindano hayo, huku Argentina ikiendelea na harakati za kutetea ubingwa wake kwa kufuzu hatua ya robo fainali.
Katika mchezo mwingine wa hatua ya 16 bora, Uswisi pia imefuzu robo fainali baada ya kuiondoa Colombia kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 4-3, kufuatia timu hizo kutoka sare katika muda wa kawaida na wa nyongeza.
Katika hatua ya robo fainali, Argentina itamenyana na Uswisi, huku Colombia ikiaga rasmi fainali za Kombe la Dunia 2026.
