Timu ya Taifa ya Hispania imefuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuichapa Ureno kwa bao 1-0 katika mchezo wa hatua ya 16 bora wa michuano hiyo.

Katika mchezo mwingine wa hatua hiyo, wenyeji Marekani wameaga mashindano hayo baada ya kuchapwa mabao 4-1 na Ubelgiji. Ushindi huo umeifanya Ubelgiji kufuzu hatua ya robo fainali, ambako itakutana na Hispania.