Mashabiki wa Simba SC wamefurika maeneo tofauti ikiwemo Jangwani jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusherehekea ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB, lililotwaliwa jana baada ya kuifunga Azam bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.
Tangu saa saba mchana maeneo mengi katika ya Jiji ambapo msafara ulikuwa unapita lilianza kujaa mashabiki waliovalia jezi nyekundu na nyeupe, wakiimba nyimbo za kusifia chama lao huku wakionyesha furaha ya kutwaa taji hilo.
Kutokana na umati mkubwa wa mashabiki waliotapakaa barabarani, magari ya kawaida yameshindwa kupita katika eneo hilo huku mashabiki wakilitawala kwa kuimba nyimbo za Simba na kushangilia ubingwa walioutwaa.
Eneo ambalo jana lilikuwa kitovu cha sherehe za Yanga baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC, leo limegeuka kuwa makutano ya mashabiki wa Simba waliojazana wakisubiri kuupokea msafara wa mabingwa wa Kombe la CRDB
Baada ya paredi hiyo Kombe la Simba lilifikishwa katika fukwe za Coco.

