Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa halmashauri kuu ya (CCM) Taifa Mohamed Mchengerwa (MNEC) ambaye pia ni Waziri wa afya wakati wa kufungua mafunzo maalumu kwa madiwani wa CCM Mkoa wa Pwani ambayo yamefanyika katika shule ya uongozi ya Mwalimu Julias Nyerere iliyopo eneo la kwa mfipa katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Mkoa wa Pwani.
Kwa uppande wake Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Ndg. Kiite Mfilinge amesema kwamba lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuwakutanisha madiwani hao ili kuwajengea uwezo ikiwa pamoja na kuwakumbushia kutekeleza majukumu yao pamoja na kuwahudumia wananchi.
Kwa upande wake Mwalimu wa shule ya uongozi mwalimu Julias nyerere Profesa Mercellina Chijoriga ambaye pia alikuwa mtoa mada katika mafunzo hayo amesema amebainisha kuwa mafunzo hayo yataweza kuleta tija zaidi ya uwajibikaji katika suala zima la kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.
Pia Profesa huyo ametumia mafunzo hayo kuwahimiza madiwani wa Mkoa wa Pwani kuzingatia kwa weledi na ufanisi mkubwa dira ya Taifa ambayo itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kutimiza majukumu yao ipasavyo ikiwemo suala zima la utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Nao baadhi ya madiwani ambao wamehudhuria katika mafunzo hayo akiwemo Ally Simba Diwani wa Kata ya Misusugu pamoja na Diwani wa Kata ya Mwewe omary Msombwe wameahidi kwenda kuyatumia vema mafunzo hayo ambayo wameyapata na kwamba yameweza kuwajengea uwezo mkubwa katika kutekeleza majukumu yao.
Mafunzo hayo ya siku moja yamewajumuisha madiwani wote wa Mkoa wa Pwani waoatao 185 ambapo wamepata fursa ya kujifunz amada mbali mbali ikiwemo suala la uzalendo, ulinzi na amani, uwajibikaji kwa wananchi wao , jinsi ya kusimamia mapato, na kujifunza mambo mbali mbali amabyo yataweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika maeneo yao.

