Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mbeya Bi. Erica Yegella amebainisha kwamba katika ziara hiyo wameambatana na baadhi ya watendaji pamoja na madiwani mbali mbali kwa lengo la kuweza kwenda kujifunza mafunzo mbali mbali kwa kioindi cha siku nne ambayo yataweza kuwasaidia katika suala zima la utekelezaji wa majukumu yao ya kikazi ya kila siku.
Yegella amesema kwamba lengo kubwa la Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuwahudumia wananchi wake na kuleta chachu ya maendeleo na mabadiliko makubwa katika nyanja mbali mbali hivyo ana imani kwamba kufanyika kwa ziara hiyo kwa upande wa madiwani itawezamkuleta tija na mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kutokana na mafunzo ambayo watajifunza.
“Nashukuru sana mimi pamoja na baadhi ya waatendaji pamoja na madiwani wangu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya tumefika salama na tumepokelewa vizuri sana Zanzibar na kwamba tumekuja maalumu kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku nne ambapo tutakuwepo katika maeneo mabali mbali ya Unguja na wenyeji wetu akiwemo Mkurugenzi mtendaji wa mjini magharibi ametupokea kwa heshima zote,”amebainisha Bi. Yegella.
Kadhalika Mkurugenzi huyo amesema katika ziara hiyo wataweza kupata fursa ya kujifunza masuala mbali mbali na kubadilishana uzoefu katika kutekeleza majukumu yao ikiwe pamoja na kutembelea miradi mbali mbali ya maendeeleo kwa ajili ya kujifunza jinsi wanavyoweka mikakati katika kutekeelza miradi hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya mjini Magharibi Bi. Sabra Machano amesema kwamba amefarijika sana na ujio wa ziara hiyo kutoka kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya na kuahidi kuwapa ushirikiano wa hali na mali katika kipindi chote watakapokuwa katika ziara ya mafunzo hayo.

