Na Mwandishi wetu,Unguja
Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya katika kuongeza jitihada za kuweza kuongeza ufanisi mkubwa  katika saula zima la uwajibikaji na kujinza mambo mbali mbali imeamua  kwenda kufanya ziara maalumu ya  kikazi Zanibar katika visiwa vya eneo la  Unguja ambayo itaweza  kuwasaidia watendaji pamoja na madiwani katika kuongeza weledi na utekelezaji wa majukumu yao mbali mbali ya kila siku.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mbeya  Bi. Erica Yegella amebainisha kwamba katika ziara hiyo wameambatana  na baadhi ya watendaji pamoja na  madiwani mbali mbali  kwa lengo la kuweza  kwenda kujifunza  mafunzo mbali mbali kwa kioindi cha siku nne ambayo yataweza kuwasaidia katika suala zima la utekelezaji wa majukumu yao ya kikazi ya kila siku.

Yegella amesema kwamba  lengo kubwa la Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuwahudumia wananchi wake na kuleta chachu ya maendeleo na mabadiliko makubwa katika nyanja mbali mbali hivyo ana imani kwamba kufanyika kwa ziara hiyo kwa upande wa madiwani itawezamkuleta  tija na mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kutokana na mafunzo ambayo watajifunza.

“Nashukuru sana mimi pamoja na baadhi ya waatendaji pamoja na madiwani wangu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya tumefika salama na tumepokelewa vizuri sana Zanzibar na kwamba tumekuja maalumu kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku nne ambapo tutakuwepo katika maeneo mabali mbali ya  Unguja na wenyeji wetu akiwemo Mkurugenzi  mtendaji wa mjini magharibi ametupokea kwa heshima zote,”amebainisha Bi. Yegella.

Kadhalika Mkurugenzi huyo  amesema katika ziara hiyo wataweza kupata fursa ya kujifunza masuala mbali mbali na kubadilishana uzoefu katika kutekeleza majukumu yao ikiwe pamoja na  kutembelea miradi mbali mbali ya maendeeleo kwa ajili ya kujifunza jinsi wanavyoweka mikakati katika kutekeelza miradi hiyo.

Kwa   upande  wake Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya mjini  Magharibi  Bi. Sabra Machano amesema kwamba amefarijika sana na ujio wa ziara hiyo kutoka kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya na kuahidi kuwapa ushirikiano wa hali na mali katika kipindi chote watakapokuwa katika ziara ya mafunzo hayo.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya BI. Aiddah Haule amesema kwamba mafunzo ambayo watayapata wakiwa katika visiwa hivyo vya unguja yeye pamoja na jopo la madiwani pamoja na mkurugenzi wapo yatakuwa ni mkombozi mkubwa katika kuleta mageuzi katika nyanja mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wananchi katika maeneo yao mbali mbali.