Na Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog, Bungeni Dodoma

‎Serikali imetumia Shilingi trilioni 1.4 kugharamia ununuzi wa bidhaa za afya kupitia Bohari ya Dawa nchini (MSD) katika kipindi cha mwaka 2021/2022 hadi Machi 2026.

‎Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo , Mei 11, 2026,  bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema kuwa fedha hizo zimetumika kununua dawa za UKIMWI, malaria, kifua kikuu pamoja na bidhaa nyingine za afya.

‎Aidha, amebainisha kuwa Serikali imewezesha kuanzishwa kwa viwanda vipya 11 vya dawa na vifaa tiba nchini.

‎Pia ameongeza kuwa Serikali imeanza kufufua kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industry kilichopo Arusha kwa ajili ya kuzalisha dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI.

‎Amesema kuwa hali ya upatikanaji wa bidhaa muhimu za afya imeongezeka kutoka asilimia 58 hadi asilimia 88.8 mwezi Machi 2026.

‎Aidha amesema kuwa TMDA imeendelea kushikilia cheti cha utambuzi wa ubora wa dawa kwa kiwango cha kimataifa cha WHO Maturity Level 3.