Na Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog, Bungeni Dodoma
Serikali imetumia Shilingi trilioni 1.4 kugharamia ununuzi wa bidhaa za afya kupitia Bohari ya Dawa nchini (MSD) katika kipindi cha mwaka 2021/2022 hadi Machi 2026.
Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo , Mei 11, 2026, bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema kuwa fedha hizo zimetumika kununua dawa za UKIMWI, malaria, kifua kikuu pamoja na bidhaa nyingine za afya.
Aidha, amebainisha kuwa Serikali imewezesha kuanzishwa kwa viwanda vipya 11 vya dawa na vifaa tiba nchini.
Pia ameongeza kuwa Serikali imeanza kufufua kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industry kilichopo Arusha kwa ajili ya kuzalisha dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI.
Amesema kuwa hali ya upatikanaji wa bidhaa muhimu za afya imeongezeka kutoka asilimia 58 hadi asilimia 88.8 mwezi Machi 2026.
Aidha amesema kuwa TMDA imeendelea kushikilia cheti cha utambuzi wa ubora wa dawa kwa kiwango cha kimataifa cha WHO Maturity Level 3.
