Na Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog, Bungeni Dodoma
Serikali imeendelea kuajiri wataalamu mbalimbali katika Sekta ya Afya ambapo jumla ya wataalamu 53,633 wameajiriwa kuanzia mwaka 2021 hadi Machi 2026.
Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kuwa wataalamu hao wamesambazwa katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini ili kuimarisha utoaji wa huduma.
Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo , Mei 11, 2026, bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa amebainisha kuwa watumishi 9,039 wameajiriwa kwa mikataba ya muda mfupi kupitia mapato ya ndani ya vituo vya afya.
Pia ameongeza kuwa Serikali imeanzisha Programu ya Samia Health Super Specialization Scholarship kwa ajili ya kuongeza wataalamu bingwa na bingwa bobezi.
Amesema kuwa wataalamu 2,982 wamepata mafunzo ya ubingwa na ubingwa bobezi kuanzia mwaka 2021/2022 hadi Machi 2026.
Aidha amesema kuwa hatua hiyo imeongeza uwezo wa utoaji wa huduma za ubingwa nchini na kupunguza utegemezi wa matibabu nje ya nchi.
