“Asiyehusika yoyote atae mbali na Uwanja wa Mkapa, najua tunaumia hata mimi mwenyewe naumia.”
“Kwa kuwa watu wanataka kuiona timu yao pamoja kama tulivyozoea, mdhamini wetu wa michuano ya kimataifa akaona atuandalie kitu cha kutuweka pamoja. Mo Cola ametutengea eneo maalumu la kukutana kuona timu yetu na eneo lenyewe ni Mwembe Yanga lililopo Temeke. Tutakuwepo pale kuanzia saa 5 asubuhi na kutakuwa na screen kubwa vibaya mno, hamjawahi kuiona.”
“Kutakuwepo na burudani mbalimbali siku hiyo kama mwimbaji wa nyimbo ya Wivu ambaye ni Dj Mushizo lakini pia atakuwepo Dj Sinyorita.”
“Lakini pia wiki mbili ziliopita tulizindua kampeni ya Onja na Ushinde ukinywa Mo Cola. Hivyo siku ya Jumapili Januari 19, 2025 kutakuwa na zoezi la kugawa zawadi kwa washindi na wengine watashinda pale pale.”
“Mimi binafsi Jumapili sitaenda uwanjani, taenda Mwembe Yanga. Nimeshazoea kelele hivyo takuwa na Wanasimba wenzangu kufurahia.”
“Kampeni ya Tunawajibika Pamoja hadi sasa tuna milioni 47,141,024.“- Ahmed Ally.