Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam unatarajiwa kuwa mwenyeji wa michezo yote miwili ya Simba SC na 15 de Agosto ya Equatorial Guinea katika Raundi ya Pili ya Kufuzu Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF Champions League), baada ya klabu hiyo ya Equatorial Guinea kuchagua uwanja huo kuwa uwanja wake wa nyumbani.

Uamuzi huo unamaanisha kuwa Simba SC na 15 de Agosto zitakutana mara mbili katika uwanja huo huo, hali itakayowapa mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi fursa ya kushuhudia michezo yote miwili jijini Dar es Salaam.