Meneja wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Tanganyika(TPA) Kigoma , Bw. Ajuaye Kheri Msese akitoa maelezo kwa waandishi wa habari walipotembelea katika bandari ya Kigoma Ziwa Tanganyika leo.
…………………………………………………
Meneja wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Tanganyika(TPA) Kigoma , Bw. Ajuaye Kheri Msese amesema Bandari ya Kigoma inayo miradi mikubwa mitatu inayotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 32.5 ambapo utekelezaji wa miradi hiyo umefikia asilimia 15%.
Bw, Msese ameongeza kuwa miradi inayotekelezwa ni Gati za bandari za Kibirizi, Ujiji na Ofisi ya Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Kigoma inayosimamia bandari za ziwa Tanganyika.
Msese ameongeza kuwa Ujenzi huo unahusisha usanifu na ujenzi wa gati za Kibirizi na Ujini pamoja na ofisi ya Meneja Mkuu wa Bandari Kigoma na ujenzi wa miradi hiyo unafanywa na kampuni ya ujenzi ya China Railway 15 Group Corporation (CR15G) ya China.
Ameongeza kuwa katika mradi wa Gati ya Kibirizi utahusisha ujenzi wa Maghala matatu ya kuhifadhia mizigo, Jengo la abiria, Uzio kuzunguka bandari pamoja na ofisi ambayo itahusisha idara zote muhimu kama vile Uhamiaji, Polisi na TRA kwa sababu tunapakana na nchi jirani kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Burundi na Zambia hivyo wageni mbalimbali kutoka nje lazima wapitie katika bandari zetu za ziwa Tanganyika.
Amesema awali wananchi walikuwa wakipata tabu sana ili kupanda kwenye maboti waliyokuwa wakisafiria, hivyo kama bandari walifanya jitihada kuhakikisha wanajenga gati za muda kwa kuweka maboya kabla ya kukamilika kwa mradi huu wa gati Kibirizi na Ujiji ili wananchi waweze kupanda na kupakia mizigo yao kwenye boti bila tabu ya kuingia kwenye maji.
Akizungumzia uwepo wa Bandari Bubu katika ziwa Tanganyika Msese amesema “Mamlaka ya Bandari ipo katika uchambuzi wa taarifa kuhusu bandari bubu ili zirasimishwe au kufungwa kwa zile ambazo hazipo kwa mujibu wa sheria ili zifanye kazi kulingana na kanuni na taratibu za sheria.
Msese anamaliza kwamba “Kufanyika kwa uchambuzi huu kutaimarisha ulinzi na usalama kwenye mipaka na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa pamato ya katika bandari zetu”.
Naye Ofisa Mwendeshaji wa Bandari ya Kibirizi Bw. Ghalib Mhyoro kifafanua jambo kwa waandishiwa habari walipotembelea bandari ya Kibirizi mjini Kigoma.
Baadhi ya abiria wakiwa kwenye boti tayari kwa kuanza safari.
Boja ya boto zinazosafirisha abiria kutoka bandari ya Kibirizi mjini Kigoma ikiopakia abiria.
Baadhi ya boti za abiria na mizigo zikiwa zimeegeshwa katika bandari ya Kibirizi ziwa Tanganyika.