Home Mchanganyiko ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUMBAKA MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE

ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUMBAKA MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE

0

*************************************

Tukio la Kwanza

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAMSHIKILIA KIJANA MMOJA
AITWAYE MICHAEL MAYALA, MIAKA 16, MKAZI WA KISHINDA KWA
TUHUMA ZA KUMBAKA BERTHA JOSEPH, MIAKA 13, MWANAFUNZI
WA DARASA LA NNE HUKU AKIWA AMEMZIBA MDOMO NA PUA KWA
KANGA HADI KUPELEKEA KUPOTEZA MAISHA, KITENDO AMBACHO
NI KINYUME NA SHERIA TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 05.06.2016 HUKO KATIKA KIJIJI CHA KISHINDA, WILAYA YA SENGEREMA, HII NI BAADA YA
MTUHUMIWA HUYO AKIWA NA BINAMU YAKE (MAREHEMU) NA
NDUGU ZAO WENGINE WAWILI WANAOISHI WOTE HAPO KIJIJINI
KWA BIBI YAO WALIKWENDA SHAMBANI KUPALILIA MATUTA
AMBAPO KILA MMOJA ALITAKIWA KUPALILIA MATUTA MATANO(5).

AIDHA, WENZAO WAWILI WALIMALIZA NA KUTANGULIA NYUMBANI
WAKABAKI MTUHUMIWA NA MAREHEMU WAKIMALIZIA KAZI NDIPO
MTUHUMIWA ALIMKAMATA MAREHEMU NA KUMZIBA MDOMO NA
PUA KWA KUTUMIA KANGA ALIYOKUWA AMEVAA MAREHEMU KISHA
KUMBAKA NA KUPELEKEA MAREHEMU KUPOTEZA MAISHA PAPO
HAPO.

BAADA YA TUKIO HILO MTUHUMIWA ALIRUDI NYUMBANI NA
ALIPOULIZWA NA WAZAZI KUWA MWENZAKE YUKO WAPI ALIJIBU
KATANGULIA KURUDI NYUMBANI, NDUGU WALIANZA KUMTAFUTA
MAREHEMU BILA MAFANIKIO NDIPO MTUHUMIWA ALITOROKA
NYUMBANI KWENDA KIJIJI CHA KATUNGURU KWA NDUGU ZAO
WENGINE, FAMILIA ILIMTILIA MASHAKA NA BADAE WALIMKAMATA
NA KUMPELEKA POLISI ALIPOHOJIWA ALIKUBALI KUHUSIKA NA
TUKIO HILO NA KUWAPELEKA POLISI HADI SHAMBANI ENEO MWILI
WA MAREHEMU ULIPOKUWA.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA NA MAHOJIANO
NA MTUHUMIWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA
MAHAMANI. MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA
UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU KWA AJILI YA MAZISHI.

Tukio la Pili;

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAMSHIKILIA JOHN
SAMWELI, MIAKA 18, MKURYA, MKAZI WA IBANDA, KWA TUHUMA
ZA KUMLAWITI MTOTO WA KIUME JINA TUNALIHIFADHI, MWENYE
UMRI WA MIAKA MIWILI NA NUSU NA KUMSABABISHIA MAUMIVU
MAKALI SEHEMU ZA SIRI, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 10.06.2019 MAJIRA YA SAA 13:00HRS
HUKO MAENEO YA IBANDA KATA YA KIRUMBA WILAYA YA
ILEMELA, HII NI BAADA YA MTUHUMIWA KUMCHUKUA MTOTO NA
KUMRUBUNI KUWA ANAKWENDA KUMNUNULIA SODA NDIPO
WALIPOFIKA VICHAKANI ALIBADILIKA NA KUMTENDEA KITENDO
HICHO CHA KIKATILI.

HATA HIVYO, WAKATI MTUHUMIWA ANAENDELEA KUTENDA
UNYAMA HUO. MTOTO ALIKUA AKIPIGA KELELE AKIOMBA MSAADA,
WATU WALISIKIA NA KWENDA KUMSAIDIA NDIPO WALIMKUTA
MTUHUMIWA AKIWA ANAMLAWITI MTOTO. WANANCHI WALITOA
TAARIFA POLISI NDIPO ASKARI WALIFIKA KWA HARAKA ENEO LA
TUKIO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA.

JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA
PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
MTOTO AMEPELEKWA HOSPITALI YA MKOA SEKOU TOURE
KUPATIWA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINATOA ONYO KWA BAADHI
YA VIJANA WENYE TABIA CHAFU NA YA KIKATILI YA
KUBAKA/KULAWITI KUWA WAACHE KWANI NI KINYUME NA SHERIA
NA ENDAPO MTU/WATU WATABAINIKA HATUA KALI ZA KISHERIA
ZITACHUKULIWA DHIDI YAO.