Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna akizungumza na wateja hao walipotembelea Makao Makuu ya NMB kujionea shughuli mbalimbali za kibenki zinazofanyika hapo
Mkuu wa Huduma Jumuifu –
Nenyuata Mejooli akizungumza na wateja.
Afisa Mkuu Uendelezaji wa Bidhaa na Matumizi ya Digitali NMB – Pete Novat akizungumza na wateja
Mkuu wa Biashara Wateja Wadogo na wa Kati wa NMB –
Filbert Mponzi katika picha ya pamoja na wateja walipotembelea Makao Makuu ya NMB.
…………………………………………
Wafanyabishara wadogo wameziomba taasisi za fedha kuwawezesha ili waanzishe viwanda na kupunguza safari za China kufuata bidhaa ambazo zingeweza kuzalishwa nchini.
Hayo yameelezwa na wajasiria mali 10 waliohudhuria kongamano la biashara nchini China chini ya ufadhili wa benki ya NMB.
Wajasiriamali hao wameeleza kuwa katika ziara hiyo wamebaini China ina viwanda vidogo vidogo vingi ambavyo ndivyo vinazalisha bidhaa wanazotumia gharama kubwa kuzifuata au kuagiza.
Mmoja wa wajasiriamali hao Arnod Mapunda anayejihusisha na uuzaji wa vifaa vya pikipiki amesema kinachowagharimu watanzania ni bidhaa nyingi kununuliwa nje ya nchi.
Amesema ziara hiyo imemuzesha kutambua kuwa inawezekana kuanzisha kiwanja kidogo na ukapata matokeo makubwa.
“Vyote tulivyooona huko vinawezekana endapo tutaamua na hili walione wenzetu wenye taasisi za fedha, wawakopeshe wajasiriamali ili waweze kufanya uwekezaji tupunguze kuagiza kutoka nje,” amesema Mapunda
Naye mfanyabiashara wa maziwa mkoani Morogoro, Rehema Mmari amesema kupitia ziara hiyo ameweza kupata mawazo kadhaa ya biashara ambazo anaweza kuzifanya akipata fedha za kutosha.
Amesema, “ Nimefikiria biashara ya nywele maana nimeona mashine ya kutengeneza na vitu vingine vingi vizuri, hakuna sababu ya kununua mzigo nje ya nchi tukiwa na viwanda vidogo hapa nyumbani tunaweza kabisa,”
Kwa upande wake Mkuu wa biashara wa NMB, Donatus Richard amesema waliamua kuwawezesha wafanyabishara hao kuhudhuria kongamano hilo ili wakajifunze kutoka kwa wafanyabishara wa China namna wanavyoendesha biashara zao.
Sanjari na hilo ziara hiyo ililenga kujifunza ni namna gani wanaweza kufanya uwekezaji wenye tija hapa nchini ili kupunguza safari za kwenda China.
“NMB huwa tuna klabu za wajasiriamali ‘NMB Business Club’ tunawafundisha masuala mbalimbali ya biashara, mwaka huu tukaona twende mbele tukawapeleka China wakajifunze zaidi kwa kujionea,”
“Wametembelea viwanda na kuhudhuria kongamano la bishara ni matumaini yetu wamejifunza vingi na watafundisha wenzao kile walichojifunza, maana wametoka katika mikoa ya kanda zote nane,” amesema Richard
Ziara hiyo ya siku 10 ilianza Oktoba 13 na kuhitimishwa Oktoba 23.