Home Michezo NYASA DC YAIZAMISHA 6-0 NANGOMBO FC LIGI YA UCHAGUZI CUP

NYASA DC YAIZAMISHA 6-0 NANGOMBO FC LIGI YA UCHAGUZI CUP

0

Timu ya mpira wa miguu ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, jana imeibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya timu ya Nangombo fc, zote za Wilayani hapa katika mchezo wa ligi ya “Uchaguzi Cup” yenye lengo la kuhamasisha wananchi wa Wilaya ya Nyasa kushiriki kikamilifu katika  uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Ligi hiyo imeanzishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Bi Isabela Chilumba ambayo inashirikisha Timu kumi na mbili kutoka Wilayani hapa.

Wafungaji katika mechi hiyo ni filbert  Mpangala aliyefunga dakika ya 5 na 12, wakati gerold Mwela akifunga dk ya 25 na dakika ya 44 Hashimu alifunga bao la nne ,mpaka timu zinaenda mapumziko Timu ya halmashauri ya Nyasa 4 nangombo fc  0.

Kipindi cha pili timu zote zilianza mpira kwa kushambuliana kwa zamu lakini jahazi la Nangombo lilizidi kuzama pale kibo alipofunga magoli 2 dakika ya 67 na 82. Mpaka Mpira unakwisha nyasa dc fc 6 Nangombo 0

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa alisema amefurahi kuhudhuria mchezo huo na amepata burudani nzuri, na kuwataka watumishi na wananchi wote wa Wilaya ya Nyasa kuhamasika kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika novemba 24 ili wachague viongozi wanaowapenda.

Akizungumza na wachezaji wa timu zote mbili mara baada ya mpira kumalizika Mkuu wa wilaya ya Nyasa ameipongeza timu ya Halmashauri ya wilaya ya nyasa kwa ushindi,pia ameeipongeza Timu ya Nangombo kwa kucheza vizuri licha ya kufungwa kwa kuwa lengo la mashindano hayo ni kuwahamasisha wananchi kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 Mwaka huu.