SHULE ya Msingi Atlas Madale, imeinyuka shule ya Msingi Atlas iliyopo Ubungo bao tano kwa sifuri katika mchezo wa soka uliochezwa katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Atlas iliyopo eneo la Mivumoni, Madale Wilayani Kinondoni.
Mchezo huo wa kirafiki ulichezwa katika bonanza maalum baina ya shule hizo mbili kwa wanafunzi wake wa Darasa la saba kutokea shule ya Atlas iliyopo Ubungo na wa sekondari kutoka Shule ya Atlas iliyopo Madale zote zinamilikiwa na kampuni ya ‘Atlas Mark Group’ ya Jijini Dar es Salaam.
Mabao hayo matano yalifungwa na wachezaji machachari ambao ni Paul Njowoka, Petro Njowoka, Ally Salum, Ostrak Komba na Nassir Juma wote wa darasa la saba.
Aidha mchezo kati ya kidato cha kwanza na darasa la saba, darasa la saba waliibuka kidedea kwa bao mbili kwa moja huku mchezo kati ya kidato cha nne na cha tatu kidato cha tatu walishinda kwa penati 5. kabla ya hapo timu hizo zilikuwa nguvu sawa kwa bao moja kwa moja.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuu wa shule ya Msingi ya Atlas iliyopo Ubungo, Justus Kagya anasema kuwa bonanza hilo lililowakutanisha wanafunzi wa darasa la saba wanaotegemea kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi mwezi Septemba mwaka huu na wale wa Sekondari ya Atlas iliyopo Madale ni mkakati wa kuboresha mahusiano baina ya wanafunzi wa shule hizo mbili na kuwaandaa kitaaluma wale wanaotarajia kumaliza darasa la saba mwaka huu.
“Huu ni mwanzo tu, tutakuwa na shughuli mbali mbali za kimichezo na kitaaluma ili kuwaandaa wanafunzi wetu wa darasala la saba kuzoea mazingira ya sekondari pia kuwaandaa kisaikolojia juu ya maisha ya kitaaluma wanayotegemea kukutana nayo hapo baadae.
Kyaga anasema kuwa mbali ya mchezo wa soka,vile vile kulikuwepo na usomaji wa mashairi, mijadala mbali mbali kwa nia ya kuboresha lugha miongoni mwa wanafunzi, kutanua uelewa wao na kujenga ujasiri miongoni mwao.
Makamu Mkuu wa shule ya sekondari Atlas upande wa taaluma, Moses Reuben anasema shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 352 iliyoanza mnamo mwaka 2015, sasa inatarajia kutoa wanafunzi wa kidato cha nne kwa awamu ya pili.
Akitolea mfano wa matokeo ya kidato cha pili kuanzia mwaka 2016 anasema, mwaka 2016 kulikuwepo jumla ya wanafunzi 46, kati yao 44 walipata divisheni one na wawili divisheni two, mwaka 2017 walikuwepo jumla ayw anafunzi 88, kati yao 83 walipata divisheni 1, huku watano wakipata divisheni 11 huku mwaka 2018 jumla ya wanafunzi 136 walifanya mtihani wa kidato cha pili na kati yao wanafunzi 116 walipata divisheni 1 na kumi kati yao walipata divisheni 11.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, kiwanjani hapo, mwanafunzi wa darasa la saba kutoka shule ya Atlas iliyopo Ubungo Kelvin Godwin anasema amevutiwa sana na mazingira yaliyopo shule ya sekondari Atlas na anatamani akimaliza elimu ya darasa la saba aweze kujiunga na shule hiyo ndugu na anayomaliza sasa.
“Mazingira ni mazuri mno, nimependa kuna uwanja mkubwa wa kuchezea, mazingira yametulia kwa ajili ya kujisomea, natamani kuja huku sekondari” anasema Richardson Richard Paschal wa darasala la saba shule ya Atlas iliyopo Ubungo.
Jumla ya wanafunzi 248 wanatarajia kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu kutoka shule ya Atlas iliyopo Ubungo na wengine 392 kufanya mtihani wa darasa la nne shuleni hapo.
katika shule ya msingi Atlas Madale, jumla ya wanafunzi 355 wanatarajia kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu.