Mwanachama wa chama cha Tanganyika Afrikani National Union (TANU ) mzee Omary Nzowa mkazi wa mkoa wa Iringa akionyesha picha ya wanachama wa TANU mkoa wa Iringa ambao wengi wao wamekwisha fariki dunia ,jana wakati akizungumza na wanahabari (picha na Francis Godwin.

***************

NA  FRANCIS GODWIN, IRINGA

Mwanachama  wa  chama  cha Tanganyika  Afrikani  National Union (TANU )  mzee Omary  Nzowa  mkazi  wa  mkoa  wa  Iringa  amewataka vijana   nchini  kuwa  wazalendo na  Taifa kama  ilivyokuwa kwa vijana  wa enzi  za TANU  ambao  hawakutanguliza maslahi yao  mbele katika  kulitumikia Taifa .

Akizungumza na  mwandishi wa habari  hizi jana  ofisini  kwake Nzowa alisema  kuwa  wakati  wa  chama  cha  TANU  vijana na wachama  wote  walijitolea  mali  zao  kwa  ajili ya  chama na chama  hicho  kilikuwa na  heshima  kubwa  na hata kama dini zingechelewa  kufika basi watanzania  wote  dini  yao  ingekuwa na TANU tofauti na  sasa watu  kutanguliza maslahi mbele badala ya  uzalendo.

“ Heshima  kubwa iliyokuwepo kwa wanachama wa TANU na imani  kubwa walioonyesha  kwa chama  hicho na uzalendo  waliokuwa nao  TANU ingekuwa ni  dini ya  watanzania kama  dini   zilizopo  sasa  zisingeingia nchini  nataka  kusema  kuwa  mwanachama wa TANU  ukitembea na kadi yako  ulikuwa unaheshimika na hata  ukisafiri  kwenye basi  kama huna nauli  ukionyesha kadi  abiria  wanakuchangia nauli yako “alisema

Kwa  sasa  hali  hiyo ya uzalendo na kuheshimiana  inazidi kushuka kwani   watu  wametanguliza  mbele maslahi yao badala ya  uzalendo na ujamaa .

“ Ukiniambia  nielezee ugomvi  uliopo sasa na hali  iliyopo  sasa nchini ni ugomvi wa maslahi lakini  wato  walijitolea  mali zao  walijitolea nyumba  zao kwa ajili ya chama  cha TANU na hakukuwa na malipo  yoyote kuanzia  katibu  hadi  chini ilikuwa ni bure  kujitolea “ alisema  Nzowa

Kuwa  kwa sasa ni  wakati tofauti  sana na dunia imebadilika kwa chama kuwa maslahi  hivyo  kuna haja  kubwa  sana ya kueneza umoja wa watanzania  hasa  ukizingatia sasa  kizazi   kilichoanzisha  TANU  si kizazi  kilichopo sasa  kwani  kizazi kile cha TANU   kilikuwa na  utayari kwa sababu  wameuona  utawala wageni wakoloni ndio maana  walikuwa na mshikamano .

Nzowa  alisema  kuwa  maombi yake kwa watanzani  kuonyesha  mshikamano  wa  kizalendo   kwa  sasa  kwa  sababu  hata  vijana  wengi  wametembea na  kuona  na hata  ukiwauliza leo  utawasikia  wakisema  kuwa Marekani na Uingereza hawafanya kama  sisi  wanataka   Taifa  kuendelea  kutawaliwa kwa  kuwa kutawaliwa si  bendera  bali hata  mawazo  ya   kutoipenda  nchi yako ni  wazi kwa  vijana wenye  mawazo hayo ni  wale  wasio na  uzalendo .

“ Ushauri  wangu kwa vijana  ambao  wanapenda  kutolea  mifano ya mataifa mengine  badala ya  kutanguliza uzalendo  kujaribu  kuwatafuta  wazee  walioopata  kuona utawala  uliopita  na  kufuatilia maisha ya  wanachama  wa TANU  jinsi walivyoishi  kizalendo na  kudumu na mawazo   hayo kama  njia ya kulifanya Taifa la  kizalendo “

Nzowa  akizungumza  huku  akionyesha  picha iliyopigwa  enzi za TANU na  wanachama wa TANU  mkoa wa Iringa alisema katika picha  hiyo yenye  zaidi ya watu 10 wanachama  wa TANU ni mwanachama mmoja pekee  ambae ni hai na kuwa mwanachama huyo  alipata  kuwa  mkuu wa wilaya  na mkuu wa mikoa mbali mbali  ila  wapo  wanachama kama  mzee Mohamed Amer Abri ukiangalia sasa  kupitia  kizazi  hicho kuna wajukuu  zake akina Salim Abri ni mjumbe wa Halmashauri  kuu ya CCM Taifa (NEC) mkoa  wa Iringa na Arif Abri ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa .

Kuwa misingi ya bora  ya uzalendo   kwa  familia ambazo   zimetokana na TANU  ambazo  ni  chache  imeendelea  kulifanya  Taifa   kuwa imara  japo  kuna haja   uzalendo  huo  kuenezwa  zaidi kama njia ya kulifanya Taifa  kuishi kama  enzi  za TANU.

“ Ushahidi  wa  picha  hii  na  eneo  ilipopigiwa ndipo  ilikuwa ofisi ya TANU Iringa na huyu  mzee Mohamed Abri   ni mzee  ambae  alijichanganya  na wananchi na familia nzima ilikuwa imejichanganya  na wananchi na  kwenda pamoja katika  kutafuta  uhuru wa nchi  yetu  na nyumba  hii iliyoanzia TANU mwenyenyumba  alikuwa akiitwa  Omray Albart ambae  amekwisha kufa  ila baada ya  chama kuondoa ofisi hapo  nyumba hiyo iliuzwa  ila ushauri wangu kwa  vijana  uzalendo nin itikadi na ukiwa mzalendo utapenda  kujua historia  ya akina nani ambao  walipingania  nchi  kufika hapa “  alisema Nzowa

Kuwa  kama vijana  watatanguliza uzalendo  badala ya maslahi   nchi  hii itazidi  kuheshimika   daima na  wazee  wataendelea  kuheshimika  kwani nchi  ilipofikia kwa sasa wapo watu ambao  waliifanya  iwe hivi  sasa kwani walipoteza mali zao na  utu  wao  kwa ajili ya  kuona  nchi  imepata  uhuru .

“ Uhuru  huu umepatikana kwa  uvumilivu  mkubwa na watu  kujitolea  na  uhuru haukupatikana kwa  urahisi  ila ulipatikana  kwa watu  kujitolea  na kipimo cha  juu  ni  kuwa mzalendo na Taifa  kuwa  vijana wengi  wanatanguliza maslahi  ila  kama  wanachama wa TANU nao  wangetanguliza maslahi  nchi  hii isingekuwa hapa ilipo leo .